JAMHURI YA WAUNGWANA

Ushauri kwa Rais Magufuli

Ndugu Rais, salaam. Utii wangu kwako hauna shaka yoyote tangu nilipokufahamu ukiwa mwanasiasa chipukizi, nami nikiwa mwandishi mchanga wa habari. Mapenzi yako kwa Watanzania yananishawishi nivutiwe kukuita ‘Ndugu Rais’. Ushujaa na misimamo yako si tu kwamba vilinishawishi nivutiwe na uongozi wako, bali pia vimekuwa mihimili ya imani yangu kwako kutokana na hulka uliyonayo ya kuweka maslahi ya nchi yetu mbele. ...

Read More »

Nampongeza Waziri Mkuu

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameshatimiza mwaka mmoja tangu ashike wadhifa huo. Ukimtazama usoni, unamuona Majaliwa tofauti na yule aliyeonekana siku jina lake likisomwa bungeni Dodoma kushika wadhifa huo. Huyu ni Majaliwa aliyejaa msongo wa kazi nyingi alizokubali kuzibeba kwa ajili ya kuwatumikia Watanzania. Katika kipindi chake cha mwaka mmoja, Waziri Mkuu ameonesha kuwa uamuzi wa Rais John Magufuli kumteua kushika ...

Read More »

Karibu Jenerali Waitara, jiandae kukabiliana na wanasiasa

Nimemfahamu zaidi Jenerali George Waitara wakati huo akiwa na cheo cha Brigedia Jenerali. Ukaribu wangu kwenye shughuli mbalimbali za kijeshi, uliochochewa na mapenzi yangu kwa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), ulinisaidia kumwona mara kwa mara akiwa kwenye shughuli kadha wa kadha, akimwakilisha Mkuu wa JWTZ wa wakati huo, Jenerali Robert Mboma. Nakumbuka fununu za kung’atuka kwa Jenerali ...

Read More »

Jeshi la Polisi liundwe upya

Hivi karibuni kwenye gazeti hili tuliandika habari iliyohusu mtandao wa matapeli wa madini unaowahusisha polisi kadhaa jijini Dar es Salaam. Tukaeleza kwa kina namna polisi hao wanavyoshirikiana na matapeli wa madini kuwaibia wenyeji na raia wa kigeni kutoka mataifa mbalimbali duniani. Tukaenda mbali zaidi kwa kuweka hata majina ya polisi hao na mahali walipo. Katika nchi zenye kujali maadili, habari ...

Read More »

Nimeziona barabara, hii ya Butiama ni janga!

Watanzania wangependa kuona kazi nyingi za ujenzi wa barabara zikifanywa na mandarasi wazalendo.  Rais John Magufuli, akiwa Waziri wa Ujenzi, alikuwa mstari wa mbele kuhimiza umoja, weledi na kujituma miongoni mwa makandarasi wazalendo ili waweze kufanya kazi ambazo kwa muda mrefu zimeshikwa na makandarasi wageni.  Hili ni jambo jema, na kwa kweli Serikali inayowajali watu wake, haina budi kufanya hivyo. ...

Read More »

Kumbe inawezekana

Rais John Magufuli, alipoapishwa kuongoza Taifa letu, nilisema endapo sheria za nchi zitatambuliwa, kuheshimiwa na kusimamiwa, kazi yake ya kuongoza haitakuwa ngumu. Kweli, siku chache baada ya kuingia madarakani, yapo mambo mengi mazuri aliyoyafanya kwa nia moja tu ya kuirejesha nchi kwenye mstari ili safari yetu ya maendeleo iweze kuendelea vema. Rais Magufuli, kwa hulka na kasi yake kwenye masuala ...

Read More »

Mkaa: Hata misitu sasa inalia (1)

Siku chache zilizopita, Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Misitu Tanzania (TFS), Profesa Dos Santos Silayo; na Mkurugenzi wa Mipango na Matumizi wa TFS, Mohamed Kilongo, wametangaza mpango kamambe wa kuratibu biashara na matumizi ya mkaa nchini. Taarifa ya wataalamu hao zinaonesha kuwa uharibifu wa misitu kutokana na matumizi ya mkaa ni hekta 372,000 kwa mwaka. Kiwango hiki ni sawa na ...

Read More »

‘Nateseka, walimwengu nisaidieni’

Simu yenye namba 0768 299534 inaita. Kwenye orodha ya namba nilizonazo haimo. Ni namba mpya. Napokea, na mara moja nasikia sauti ya unyonge ikilitaja jina langu. Bila kuchelewa anataja jina lake. ‘Naitwa Mangazeni, nipo hapa Butiama, naomba ndugu yangu unisaidie kufikisha kilio changu kwa walimwengu ili waweze kunisaidia.” Anaendelea: “Naomba uweze kufika hapa nyumbani kwangu uone mtoto wangu anavyoteseka. Nimemhudumia ...

Read More »

Rais Magufuli asiwaogope manabii wa wakwepa kodi

Wakati wa kudai Uhuru, wapo Waafrika waliodhani mapambano yale yasingefanikishwa na Waafrika. Waafrika shupavu kwa pamoja na Wazungu na Waasia wachache walipounganisha nguvu kuutokomeza ukoloni, bado kukawapo watu walionekana kutofurahishwa na hatua ya kujitawala! Kwa kutofurahishwa huko, wakaamua kuwa vibaraka wa maadui wa ndani na nje ya nchi yetu. Hostoria inabainisha wazi kuwa kuna Watanganyika (wakati huo) waliochukizwa na kitendo ...

Read More »

Anahitajika ‘Steven Wasira’ mwingine

Mengi yanazungumzwa. Yanailenga Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Dk. John Magufuli. Mengine yanalilenga Bunge na hapa anaguswa Naibu Spika, Dk. Tulia Ackson. Haya si mambo ya kuachwa au kupuuzwa. Kuna majibu yanahitajika. Majibu yanaweza yakawa ya faragha, au ya kwenye hadhara. Baadhi ya wakosoaji wanamwona Rais Magufuli ni aina ya dikteta. Wanajadili kuzuiwa kwa mikutano ya kisiasa kana ...

Read More »

Tumefeli somo la ustaarabu

Kuna ‘kosa’ nimelitenda hivi karibuni. Kosa lenyewe ni la kuwakwida vijana wawili walioamua-bila soni- kujisaidia hadharani katika barabara tunayoitumia mtaani kwetu. Wale vijana sura zao zilikuwa ngeni kwangu. Nilipowakaribia, nilishuka katika gari na kuwauliza kwanini wameamua kujisaidia hadharani. Jibu lao likawa: “Samahani mzee”. Wakati wakijiandaa kufunga suruali zao, nikajikuta tayari nimeshawadaka. Kama wangeamua kujibanza kichakani (kumbuka walikuwa mbele ya kichaka), ...

Read More »

Video iliyonitoa machozi

Muda ni saa 3:35 usiku wa Ijumaa ya wiki iliyopita. Nimejipumzisha barazani baada ya kupambana na foleni za Dar es Salaam. Simu yangu inaashia kuingia kwa ujumbe wa WhatsApp. Nafungua na kuanza kuusoma: “Kuna njia gani ya kuwapata hawa wanaume wawili waliomtesa huyu mwanamama kiasi hiki?” Chini ya ujumbe huo, kuna ‘clip’ mbili za video zilizoambatanishwa na maneno haya ya ...

Read More »

Bado sijaona kosa la Rais Magufuli

Tukisema tunaambiwa mahaba yametuzidi. Tunaambiwa tunyamaze kwa kuwa furaha yetu ni ya muda- bado yuko kwenye honeymoon (fungate). Wapo wanaosema eti hata Jakaya Kikwete, alipoingia madarakani mwaka 2005 tulimshangilia, lakini baadaye ni sisi hao hao tuliogeuka na kuanza kumlaumu kwa uongozi wake legelegele. Wanaosema hivyo hawajakosea hata kidogo. Ni kweli wengi wetu, si tu tulimshangilia, bali tulimuunga mkono na hata ...

Read More »

Rais Magufuli angazia mafuta ya mawese (2)

Wabunge wazoefu wamelia na kuiomba Serikali isibariki “mauaji” haya kwa wakulima wetu. Wametumia kila aina ya maneno kuwashawishi wakubwa serikalini, lakini mwishowe wameshindwa. Historia itawahukumu kwa haki. Hansard zipo. Nani hawezi kuamini kuwa ushindi ambao serikali imeibuka nao bungeni umetokana na nguvu za fedha? Mbunge wa Kwela, Dk. Chrisant Mzindakaya, alizungumza vizuri sana suala la haya yanayoitwa mafuta ghafi. Akasema ...

Read More »

Wachuuzi wakiachwa hivi hivi ni ‘jeshi hatari’

Juzi nilishiriki mjadala mfupi katika mtandao wa kijamii wa Facebook. Niliweka picha ya wachuuzi waliovamia eneo la waenda kwa miguu katika eneo la Ubungo, Dar es Salaam. Maudhui ya picha hiyo yalikuwa kuwafikishia taarifa (kana kwamba hawazioni wala hawazijui) viongozi wetu juu ya hatari ya kuwapo vilio na uvunjifu wa amani katika eneo hilo. Polepole, wachuuzi wengi wameanza kuhodhi eneo ...

Read More »

Hili si shamba la bibi aliyekufa

Nimepata kuifananisha hali ya sasa ya mapambano ya kuijenga nchi yetu na ile ya nchi iliyo vitani. Taifa linapokuwa vitani, hasa vita hiyo inapokuwa halali, wananchi wazalendo huungana kuitetea nchi yao isitwaliwe na adui. Kwa wazalendo, ushindi ndiyo dhima yao kuu. Serikali ya Awamu ya Tano haiwezi kuwa ya miujiza ya kuishinda vita hii ya kimaendeleo bila ushiriki wa wananchi ...

Read More »

Hata nyegere wanaishi kwa mpangilio

Yapo mengi ambayo ningependa niwashirikishe wasomaji wa Safu hii. Wiki kadhaa zilizopita, makala yangu moja iliibua mjadala. Ilihusu Katiba mpya. Msimamo wangu si kupinga Katiba mpya, lakini bado naamini Katiba mpya pekee si suluhisho la matatizo yote yanayoikabili nchi yetu. Nitaendelea kuamini kuwa matatizo mengi ya Tanzania ni zaidi ya Katiba mpya! Hatuna viongozi wawajibikaji, na kwa sababu hiyo wananchi ...

Read More »

Mungu huyu wa M-Pesa, tiGO Pesa ananipa shaka

Wizara ya Afya imepiga marufuku matangazo ya waganga wa kienyeji na wale walioboresha neno hilo na kujiita ‘tiba mbadala’. Uamuzi wa Serikali umekuwa kama mtego wa panya – unawakamata waliomo na wasiokuwamo. Si wote wenye kutoa aina hiyo ya tiba hawafai, ila ni ukweli kwamba kuna maelfu ya matapeli walionufaishwa na umbumbumbu wetu. Miaka minne iliyopita, katika ukurasa huu huu, ...

Read More »

Tatizo la Tanzania si Katiba mpya

Mwaka 2012 niliandika makala katika safu hii iliyosema: “Nitakuwa wa Mwisho Kuishabikia Katiba Mpya”. Nilisema nimejitahidi kutafakari ni kwa namna gani Katiba mpya itatuletea mabadiliko ya kweli tunayoyataka, nimekosa majibu – na sidhani kama nitayapata. Fikra zangu zikanirejesha enzi za kudai Uhuru. Wapo walioamini kuwa kwa kupata Uhuru, taifa letu lingepiga hatua kubwa kimaendeleo. Wapo waliojiaminisha kuwa kwa kupata Uhuru, ...

Read More »

Tupigane vita hii kwa umoja

Waandishi wa habari hutakiwa wazingatie miiko na maadili ya uandishi wanapofanya kazi zao. Baadhi ya mambo wanayotakiwa kuyazingatia ni kuhakikisha wanatenda haki sawa kwa wanaowaandika. Kwa maneno mengine ni kwamba wanatakiwa watoe fursa ya kusikiliza kila upande unaoguswa kwenye habari husika. Jambo jingine, hutakiwa wasifanye kazi zao kwa upendeleo; na kwa kweli hutakiwa ‘wasiingie’ kwenye habari wanazoandika au kuzitangaza. Mara ...

Read More »

Hotuba iliyokosekana kwa miaka 10!

Kwa miaka mingi tulikosa kuisikia hotuba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania iliyojaa matumaini. Wiki iliyopita tuliisikia hotuba ya Rais akilihutubia Taifa kupitia Bunge. Wananchi waliosikiliza, waliburudika, lakini wapo wanaotia shaka. Hilo ni jambo la kawaida. Wanatia shaka wakirejea hotuba tamu kama hiyo iliyotolewa na Rais Jakaya Kikwete, Desemba 2005 katika ukumbi huo huo wa Bunge mjini Dodoma. ...

Read More »

Mwanya mwingine wa wakwepa kodi

Rais wetu sasa ni Dk. John Magufuli. Tuna wajibu wa kumsaidia ili aweze kutimiza ahadi zake nzuri alizowaahidi Watanzania wakati wa kampeni za Uchaguzi Mkuu. Kaulimbiu ya “Hapa Kazi Tu”, hatuna budi kuitekeleza kwa vitendo. Hatuna muda wa kupoteza. Uzoefu umeonyesha kuwa miaka mitano ni muda mfupi mno endapo wapiga na wapigiwa kura tutaamua kuutumia kwa malumbano. Endapo tutaamua kuanza ...

Read More »
Show Buttons
Hide Buttons