Jana ilikuwa ndiyo siku ya kuwatambulisha na kuwaapisha mawakala kwa ajili ya Uchaguzi wa Marudio Jimbo la Kinondoni, Mawakala wa CHADEMA wamekataliwa kuapishwa. Awali tulibaini tatizo hilo Kata ya Hananasif ambapo Mtendaji wa Kata aitwae Richard Supu (0655998777), aligoma kuwaapisha mawakala hao akiwataka waache majina yao hadi atakapowaita siku tatu kabla ya siku ya kupiga kura. Jambo ambalo ni kinyume cha taratibu zinazosimamia uchaguzi. Yeye amesisitiza kuwa ndivyo inavyofanyika na hawezi kufanya tofauti.

Taarifa zaidi zimeonesha kuwa karibu watendaji wa kata wote katika jimbo hilo, wamefanya hivyo kwa mawakala wa CHADEMA. Hakuna sababu yoyote ya msingi inayotolewa na wahusika kuhusu dalili hizo mbaya kabisa za kuzidi kuvuruga Uchaguzi huo. Hali hiyo ndiyo ambayo wasimamizi wa uchaguzi katika Kata ya Saranga (kati ya zile kata 43) walifanya.
Tayari chama kimewasiliana na NEC kuingilia kati suala hilo kwa haraka na kuwataka wasimamizi hao waache kutumika kufanya hila za kuharibu uchaguzi huo.
1355 Total Views 2 Views Today
||||| 0 I Like It! |||||
Sambaza!