Timu za soka za Malawi na Kenya, wiki iliyopita zilidhihirisha kulingana nguvu kwa kufungana mabao 2-2 mjini Blantyre, katika mechi ya kufuzu kucheza Fainali za Kombe la Dunia.

Malawi walianza kuongoza mabao mawili kwa moja lakini katika dakika ya mwisho, Chimango Kayira akajifunga na hivyo kupunguza matumaini ya Malawi kusonga hatua inayofuata.

 

The Flames ndio waliotangulia kufunga dakika ya 46 kupitia kwa Robion Ngalande, lakini dakika sita baadaye Mohamed Jamal akaisawazishia Harambee Stars.

 

Robert Ng’ambi alifunga bao la pili la Malawi katika dakika ya 81, kabla ya Kayira kujifunga na mechi kumalizikia.

 

Matokeo hayo yalitarajiwa kuwaweka pazuri mabingwa wa Afrika, Nigeria katika michuano hiyo.

 

Fainali za Kombe la Dunia zitachezwa mwakani nchini Brazil.

 

931 Total Views 1 Views Today
||||| 0 I Like It! |||||
Sambaza!