Na Padri Dk. Faustin Kamugisha

Watu wanaokuzunguka ni sababu ya
mafanikio. “Unakuwa na kama watu watano
ambao unatumia muda mwingi ukiwa nao.
Wachague kwa uangalifu,

” alisema Jim
Rohn. Mtazamo chanya unaambukiza.
Mafanikio yanaambukiza. Mark Ambrose
alisema: “Nionyeshe rafiki zako
nitakuonyesha wakati wako ujao.”
Ukizungukwa na watu waliofanikiwa, kesho
yako itakuwa ya mafanikio.
“Unahitaji kujichanganya na watu ambao
wanakuhamasisha, watu ambao wanakupa
changamoto kupanda juu zaidi, watu
wanaokufanya uwe mzuri zaidi. Usipoteze
muda wako wa thamani na watu ambao
hawaongezi chochote kwa kukua kwako.
Hatima yako ni jambo muhimu,

” alisema

Joel Osteen. Ukikubali kuzungukwa na watu
wenye mtazamo hasi unakuwa adui
mkubwa sana wa nafsi yako.
Usitegemee mabadiliko chanya kama
umezungukwa na watu wenye mtazamo
hasi. Mark Twain alitahadharisha. “Uwe
mbali na watu ambao wanajaribu kudharau
matamanio yako. Watu wadogo kila mara
hufanya hivyo, lakini watu wakubwa kweli
hukufanya kuhisi kuwa na wewe unaweza
kuwa mtu mkubwa.”
Baadhi ya watu wadogo watataka uwe saizi
yao au nyuma yao na hata chini yao.
Watajitahidi kukushusha. Kwa ufupi
wanakuwa na mtazamo hasi juu yako. Watu
wabaya watakushusha na watu wazuri
watakupandisha.
“Tembea na waota ndoto, waamini, watu
jasiri, wacheshi, wapanga mipango,
watendaji, watu waliofanikiwa wakiwa na
vichwa vyao kwenye mawingu na miguu
yao ardhini,

” alisema Wilfred Peterson.
Kuwa na kichwa mawinguni ni kuwa na
maono, mipango na dira. Kuwa na miguu
ardhini ni kuwa na maono au mipango
yenye uhalisia.
Pima umuhimu wa watu unaokutana nao
katika maisha yako. Nilitumiwa ujumbe huu

kwenye simu: “Wembe una makali lakini
hauwezi kukata mti; shoka lina nguvu lakini
haliwezi kukata nywele. Kila mmoja ni wa
muhimu kadiri ya lengo lake la pekee.
Usitazame chini kwa kuwadharau watu
labda kama unastaajabia viatu vyao.”
Kuna baadhi ya watu wa kawaida ambao
watakusaidia kufanikiwa. Kuna wengine
watakuonea wivu na kukukatisha tamaa,
usiwe karibu nao. “Jizungushie watu ambao
ni wazuri kweli. Nafikiri hilo ni jambo zuri,
kwa sababu watu unaojizungishia
wanakuakisi,

” alisema Aaron Rodgers.
Hakikisha unazungukwa na watu wenye
upendo, busara, hekima na wazuri wa tabia,
kwa ufupi watu sahihi, mafanikio
yatakufuata kama kivuli kimfuatavyo mtu.
Unapozungukwa na watu wema
unapunguza msongo wa
mawazo. Unapochagua watu wa
kukuzunguka kuwa mwangalifu na makini.
Simba akizidiwa hula nyasi, lakini anakuwa
mwangalifu asile miiba. Watu wengine
watapenda ulivyo navyo na si wewe.
Mwandishi wa habari siku moja alimhoji mtu
tajiri: “Sasa wewe ni tajiri, je, unawafikiria
sana marafiki uliokuwa nao wakati ukiwa
maskini?” Tajiri alijibu: “Nilipokuwa maskini
sikuwa na rafiki yeyote.” Huenda bwana

huyu marafiki aliowapata baada ya kutajirika
si watu sahihi.
“Mafanikio si chochote kama hauna watu
sahihi wa kuwashirikisha; utaishia kuwa
mpweke,

” alisema Selena Gomez.

Maisha ni mafupi hayastahili kuyapoteza na
rafiki mbaya. Mshikilie rafiki wa kweli kwa
mikono miwili. “Mtu yeyote anaweza kuwa
mzuri mbele ya uso wako, lakini inahitaji
rafiki wa kweli kuwa mzuri nyuma ya
mgongo wako,

” alisema Sam Ewing.

Ina maana kuwa rafiki wa kweli
anachokisema mbele ya uso wako ndicho
hicho anachokisema nyuma ya mgongo
wako. “Watu wengi wanataka kuwa nawe
katika gari la kifahari (Limo), lakini
unachohitaji ni mtu ambaye mtasafiri
pamoja kwenye basi wakati Limo
imeharibika,

” alisema Oprah Winfrey.

Unahitaji rafiki wa kweli ambaye hatakuacha
ukiharibikiwa.

Tamati….

939 Total Views 1 Views Today
||||| 0 I Like It! |||||
Sambaza!