Dk.Ringo Tenga wa kwanza kushoto akiwa mahakamani

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imeutaka upande wa mashtaka kuhakikisha unakamilisha upelelezi wa kesi inayowakabili vigogo wa kampuni ya mawasiliano ya Six Telecoms, akiwemo Wakili maarufu Dk.Ringo Tenga.

Mbali na Dk. Tenga, washtakiwa wengine ni mfanyabiashara Peter Noni, Mhandisi na Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni hiyo, Hafidhi Shamte, Mkuu wa fedha wa kampuni hiyo, Noel Odeny Chacha

Hakimu Mkazi Mkuu, Victoria Nongwa ameueleza upande wa mashtaka kukamilisha upelelezi baada ya wakili wa serikali, Mutalemwa Kishenyi kudai upelelezi wa kesi haujakamilika.

Kishenyi aliiomba mahakama iahirishe kesi hiyo hadi tarehe nyingine kwa sababu ya upelelezi kutokamilika.

Baada ya kueleza hayo, Hakimu Nongwa ameutaka upande wa mashtaka ujitahidi kukamilisha upelelezi ambapo ameahirisha kesi hiyo hadi January 9, 2018.

1677 Total Views 2 Views Today
||||| 0 I Like It! |||||
Sambaza!