Nyerere: Chama hakitakiwi kufanya kazi za Serikali

“Katika aina yoyote ya utawala wa kidemokrasia, Chama kinachoshika Serikali, hakitakiwi kufanya kazi za Serikali, na haifai kifanye vitendo kana kwamba ndicho Serikali.”

Haya ni maneno ya Baba wa Taifa letu, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

 

Mbowe: Spika analigeuza Bunge taasisi ya CCM

“Tutaliheshimu Bunge kama taasisi huru, lakini si lilivyo sasa kama taasisi ya CCM. Nje ya Bunge wote tunaheshimiana, lakini mambo yanakuwa tofauti bungeni kwa sababu ya Kiti cha Spika kutotenda haki.”

Hii ni kauli ya Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe.

 

Mukama: Wapigakura watakuuliza ulivyowawakilisha

“Baada ya miaka mitano, jumuiya zitawauliza wajumbe wake, mwenzetu tulikutuma kule, umefanya nini? Ulijiwakilisha mwenyewe au ulifikisha yale tuliyokutuma? Ulikuwa unaongea ya kwako?”

Maneno haya ni ya Katibu Mkuu mstaafu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Wilson Mukama.

 

Eleanor: Akili kubwa hujadili mawazo, sio watu

“Akili kubwa hujadili mawazo, akili za wastani hujadili matukio, akili ndogo hujadili watu.”

Haya yalinenwa na Eleanor Roosevelt, Mke wa Rais wa zamani wa Marekani, Franklin Roosevelt.

1540 Total Views 1 Views Today
||||| 0 I Like It! |||||
Sambaza!