*Ikulu kugeuzwa jumba la utamaduni

New Mexico, Mexico

Rais mteule wa Mexico, López Obrador,
uamuzi wake wa kutumia usafiri wa ndege
wa umma wiki iliyopita ulimtumbukia nyongo
baada ya kukwama ndani ya ndege
uwanjani kwa saa tatu kutokana na hali ya
hewa.
Amesema licha ya kukumbwa na tukio hilo,
msimamo wake wa kuuza ndege ya kifahari
iliyonunuliwa na rais anayemwachia
madaraka uko palepale.
López Obrador, alikwama kwenye ndege
alipokuwa akitoka Jimbo la kusini la Oaxaca
kwenda Mexico City, baada ya kunyesha
mvua kubwa.

“Sitatumia ndege ya rais,

” alisema akiwa
ameketi kwenye kiti na abiria wenzake
akisubiri hali ya hewa iwe nzuri ili ndege
ianze safari.
Kiongozi huyo wa mlengo wa kushoto
alishinda urais Julai, mwaka huu na
anatarajiwa kuapishwa Desemba.
Ndege ya kifahari ya rais wa Mexico,
Boeing 787 Dreamliner iliyogharimu dola
milioni 218.7, iliwasili Mexico miaka miwili
iliyopita baada ya kuagizwa na Rais Felipe
Calderón mwaka 2012.
Wakati huo ilitajwa kuwa ndiyo ndege ya
kisasa zaidi nzuri kuliko ndege
zinazotumiwa na viongozi wengine wa
kitaifa duniani.
López Obrador, ambaye ameahidi
kuongoza serikali iliyo makini, alikuwa
miongoni mwa mamia ya abiria waliokuwa
wakisafiri kutoka katika mji huo wa utalii.
Video zilimwonyesha akisema atafadhaika
endapo atatumia usafiri wa ndege wa
kifahari katika nchi ambayo ina umaskini
mkubwa.
“Katika hili sitabadili msimamo wangu,

alisema na kuongeza kuwa anaridhika na
hali ilivyo, na kwamba mwanasiasa

anayejikweza hawezi kudumu.
Hata hivyo, rais mteule huyo amekosolewa
na baadhi ya wananchi, wakisema alimradi
ndege imekwisha kununuliwa, hana budi
kuitumia.
Wamekielezea kitendo cha kukwama kwake
uwanjani kuwa si cha kawaida kwa kiongozi
mkuu wa nchi.
Pamoja na kuahidi kuuza ndege ya rais,
López Obrador, ameahidi kubadili kasri ya
rais kuwa kituo cha utamaduni na yeye
atakuwa akiishi katika nyumba ya kawaida.
Pia ameahidi kupunguza mshahara wa rais
na kuendesha mapambano makali dhidi ya
rushwa.

….tamati….

699 Total Views 1 Views Today
||||| 0 I Like It! |||||
Sambaza!