Wahamiaji haramu 85 raia wa Ethiopia, wamekamatwa katika eneo la Goba jijini Dar es Salaam baada ya kutelekezwa, anaripoti Mwandishi Wetu.

Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Dk. Anna Makakala, amethibitishia JAMHURI kukamatwa kwa watu hao.

Amesema Uhamiaji kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi wanaendelea kuwasaka wengine ambao taarifa zinasema bado wako mitaani.

“Tulipata taarifa kutoka kwa raia wema, tumewakamata. Tunaendelea kuwasaka walio mitaani. Tunaomba wananchi waendelee kutusaidia, lakini pia tunataka tuwapate waliohusika kuwaingiza nchini ili wafikishwe kwenye vyombo vya sheria,” amesema Kamishna Janerali Makakala.

Kumekuwapo wimbi kubwa la raia wa kigeni kukamatwa nchini wakiwa safarini kwenda Afrika Kusini. Pamoja na Ethiopia, nchi nyingine inayotoa wahamiaji haramu wengi ni Somalia.

.tamati..

945 Total Views 1 Views Today
||||| 0 I Like It! |||||
Sambaza!