Watanzania tusiwe kama Thomaso
Desemba 9, 2018 imeangukia siku ya Dominika, ni siku ya Bwana, sisi Watanganyika tumefanya kumbukumbu ya mwaka wa 57 wa Uhuru wa taifa letu. Ni fahari kubwa sana kwa sisi sote kukumbuka Desemba 9, mwaka ule wa 1961 tuliojikomboa kutoka mikononi mwa wakoloni Waingereza. Kwa wazee kama Mhesheshimiwa Balozi Job Lusinde kule Dodoma, nafikiri inakuwa…