Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amemshukuru Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kufanya kazi kubwa ya mfano katika sekta ya Nishati ambapo amesema Mkoa wa Dodoma muda si mrefu utakuwa ni kitovu cha usambazaji umeme katika mikoa mbalimbali ikiwemo Singida, Shinyanga, Tabora, Kigoma na Arusha na pia kitajengwa kituo kikubwa cha kusambaza umeme na kusimamia gridi ya Taifa.

Safari hiyo ya kuhakikisha minada yote nchini inatumia nishati safi ya kupikia, imeanzia katika Mnada wa Msalato jijini Dodoma ambapo tarehe 21 Agosti 2025, Dkt. Biteko amegawa majiko banifu kwa Mamalishe takriban 27 wanaohudumu katika mnada huo pamoja na majiko ya kuchomea nyama.