Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa, Balozi Asha Rose Migiro awasili leo Oktoba 6/2025 mkoani Mwanza kwa ajili ya mapokezi ya Mwenyekiti wa CCM Taifa na mgombea urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dkt. Samia Suluhu Hassan akiendelea na kampeni za uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba 29/ 2025.
Dkt Samia atapokelewa Mwanza Oktoba 07/2025 ambapo atazungumza na wananchi wa Kata Buhongwa akielekea Wilaya ya Misungwi na badae ataelekea Wilaya ya Sengerema na atakuwa na mkutano wa hadhara katika Uwanja wa Nyamagana Jijini Mwanza.



