Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. ๐ฆ๐ฎ๐บ๐ถ๐ฎ ๐ฆ๐๐น๐๐ต๐ ๐๐ฎ๐๐๐ฎ๐ป amesema Serikali yake anayoiongoza ya awamu ya sita imedhamiria kuanzisha Wizara kamili itakayoshughulikia masuala yote yanayohusiana na Vijana.
Akizungumza wakati akihutubia katika ufunguzi wa Bunge la 13 la Tanzania leo tarehe 14 Novemba 2025 Jijini Dodoma, Rais Dkt. Samia amesema anatarajia kuwa na Washauri wa Rais watakaomshauri kuhusu mambo ya Vijana ikiwemo changamoto zao.
โMimi na wenzangu katika Serikali tumefikiria kuwa na Wizara kamili itakayoshughulikia mambo ya Vijana”
“Tumeamua kuwa na Wizara kamili badala ya kuwa na Idara iliyo na mambo mengi”
“Vilevile nafikiria kuwa na Washauri wa mausala ya Vijana ndani ya Ofisi ya Rais.


