Waziri Mkuu Dkt. Mwigulu Nchemba leo Februari 11, 2026 amezindua uwanja wa ndege Mtemere uliopo katika kijiji cha Mloka, mkoani Pwani kwenye hifadhi ya Taifa ya Nyerere.
Uzinduzi wa uwanja huo umeenda sambamba na uzinduzi wa miradi mingine 20 (kufanya miradi 21) ikiwemo Malango ya kuingilia Hifadhini, vituo vya taarifa kwa wageni, kambi za wageni, Eneo la Kupumzikia wageni, Nyumba za wageni, Hosteli za Wanafunzi, kituo cha kufuatilia ikolojia, na vituo vya askari.
mradi huo ni sehemu ya utekelezaji wa Mpango wa Tatu wa Maendeleo wa Taifa wa miaka mitano unaolenga kukuza uchumi wa nchi yetu kupitia shughuli za utalii.












