Na Aziza Nangwa, JamhuriMedia, Dar es Salaam

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila,amelipa sh.mikioni tano kwa Glory Munisi ,aliyetapeliwa kiwanja kwa uzembe wa Mwenyekiti wa Serikali ya mtaa Kinondo kata ya Wazo.

Chalamila amemuamuru Mwenyekiti wa Mtaa wa Kinondo, Kata ya Wazo, wilayani Kinondoni, Jipson James Msukuma, kurejesha fedha za mwanamke huyo kwake baada ya kumpatia aliyedai kutapeliwa katika ununuzi wa kiwanja.

Hatua hiyo ilichukuliwa wakati alipokuwa kwenye ziara ya kikazi ya katika eneo la Nyakasangwe, ambapo alisikiliza malalamiko ya Glory Munisi aliyedai kulipia kiwanja lakini hakupatiwa umiliki halali kama ilivyokubaliwa.

“Baada ya kusikiliza pande zote na kupitia maelezo ya wahusika, na elekeza fedha zote zilizolipwa kurejeshwa mara moja,”amesema

Amesiisitiza kuwa viongozi wa mitaa wanapaswa kusimamia haki na uadilifu ,badala ya kuwa chanzo cha migogoro ya ardhi.

Aidha, aliiagiza Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kumchunguza Jipson James Msukuma ili kubaini kama kulikuwa na ukiukwaji wa taratibu au viashiria vya vitendo vya rushwa katika mchakato huo.

Mbali na agizo la kurejeshwa kwa fedha, Mkuu wa Mkoa alimpatia Glory Shilingi Milioni 5 taslimu za Kitanzania kama msaada wa dharura ili aweze kuendelea na shughuli zake nyingine, huku akionya kuwa yeyote atakayebainika kujihusisha na utapeli au matumizi mabaya ya madaraka atachukuliwa hatua kali za kisheria.

Aidha amesema ni vyema wenyeviti wa serikali za mitaa, wakasoma Sheria kwani Serikali ina wategemea kwani wasipoelewa vizuri wanafanya vibaya na lawama inakuja kwa serikali.

Katika hatua nyingine Chalanila amemtaka mkuu wa Wilaya,kuunda kamati maalum yenye weledi wakaweke kambi kwa miezi miwili kwenye kata hiyo.

Mabaraza ya kata yanatakiwa kushauri na sio kutoa hukumu . Aidha amewataka wajumbe wa mabaraza hayo kupewa semina za mara kwa mara ili kuwawezesha kuruka viunzi wasinase kwenye mitego ya wachache wenye nia ovu.

Chalamila amewataka wanaopeleka ,taarifa za migogoro wawe wakweli kwani ujane sio sababu ya kusema uongo.