Na Theophilida Felician, JamhuriMedia, Dodoma
SHIRIKA la amani nchini International Peace Infomation (IPI) limewateuwa jumla ya wabunge 320 watakaosaidia na wabunge wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania katika kuwaletea maendeleo wananchi.
Alitoa kauli hiyo Rais wa Shirika hilo Prof Wilson George Munguza baada ya kuzinduliwa kwa bunge hilo la amani mkoani Dodoma ambapo alisema kuwa limewateua wabunge hao 320 kwa lengo la kuisaidia Serikali katika kuhamasisha suala la amani na maendeleo ya wananchi kwa kushirikiana na wabunge wa majimbo waolichaguliwa na wananchi kwa Tanzania bara na Visiwani.
Alifafanua kuwa wabunge wa shirika hilo ambalo makao yake yako mkoani Dar es salaam wameelekezwa namna ya kuwahudumia kwa ukaribu wananchi kama ilivyo dhamira ya serikali na shirika hilo kwa ujumla.
Aidha alisema wabunge hao wameteuliwa kwa kufuata kanuni na taratibu za shirika na kazi yao kubwa ni kutoa elimu juu ya umumuhi wa kuitunza amani nyakati zote.
Hata hivyo aliziomba taasisi mbalimbali za serikali na binafsi kutoa ushirikiano kwa wabunge wa shirika hilo la IPI ili waweze kufanya kazi zao kwa ufanisi zaidi.






