Vipimo muhimu ambavyo wengi huvisahau – 1

Vipimo ni muhimu sana kwa maendeleo ya afya. Kupitia vipimo tunaweza kutambua
mustakabali wa afya zetu na hivyo kujiweka kwenye nafasi nzuri katika kupambana na maradhi
mbalimbali. Hivi karibuni takwimu kutoka Shirika la Afya Duniani (WHO) zilionesha kuwa idadi
ya wanaume watu wazima wanaopatiwa vipimo vya afya ni ndogo kuliko idadi ya jinsia nyingine.
Kupata vipimo sahihi, na kwa wakati sahihi ni kitu muhimu sana ambacho mtu anapaswa
kukifanya kwa afya yake. Kufanya vipimo kunasaidia kuyagundua magonjwa mapema kabla
hayajaanza kuonesha dalili, wakati ambao ni rahisi zaidi kutibika.
Magonjwa kama saratani, kisukari, yakigundulika mapema, itamsaidia mgonjwa kumuepusha
na matokeo hasi ya magonjwa hayo kama vile kusababisha kupoteza nguvu za jinsia, uwezo
wa kuona na hata vifo vya mapema.
Kupitia makala hii tutaviona baadhi ya vipimo muhimu sana ambavyo wengi hawavitilii
maanani. Lakini ukweli ni vipimo muhimu sana na vikiendelea kusahaulika, madhara yake kwa
afya ni makubwa sana.
Vipimo vya tezi dume
Ukweli ni kwamba ni wanaume wachache sana wanaofikiria kupata vipimo hivi vya tezi dume.
Mwanaume anakuwa hatarini zaidi kupata tezi dume kadri umri unavyozidi kusogea kuanzia
umri wa miaka 50 hivi.
Shirika la Afya Duniani limethibitisha kuwa tezi dume ni ugonjwa unaoua zaidi wanaume
ukiongozwa na saratani ya mapafu, na sababu kubwa ni kutopata vipimo mapema.
Habari njema ni kwamba tezi dume ni moja ya magonjwa machache ya aina za saratani
ambayo uwezekano wa kupona upo kwa zaidi ya asilimia 90 iwapo itagundulika katika hatua za
awali. Hivyo, ni vyema kufanya vipimo vya saratani mara kwa mara na hasa kuanzia umri wa
miaka 55.
Vipimo vya saratani ya utumbo mpana
Saratani ya utumbo mpana ni moja ya saratani zinazoua kwa kasi sana. Japo takwimu
zinaonesha kuwa wanaume wana nafasi ndogo zaidi ya kupata ugonjwa huu kuliko wanawake,
lakini hii haimaanishi kuwa wanaume wajisahau kuhusu saratani ya utumbo mpana, hasa
tukizingatia ukweli kuwa saratani inaweza kumpata mtu yeyote.
Mara zote saratani ya utumbo mpana inaanzia kwa kuota uvimbe mdogo ndani ya ukuta wa
utumbo na kadri vimbe hizo zinavoongezeka ndipo zinapotengeneza saratani ya utumbo
mpana.
Njia ya kuzuia saratani hii ni kuondoa hizi vimbe zinazoota mapema kabla hazijatengeneza
saratani. Na njia pekee ya kuzigundua vimbe hizi ni kupata vipimo mapema.
Inashauriwa kuanza vipimo vya saratani ya utumbo mpana mara kwa mara kuanzia umri wa
miaka 50 kwa sababu katika umri huu mtu anakuwa hatarini zaidi kupata ugonjwa huu.
Vipimo vya saratani ya ngozi
Ngozi kwa kuanza kubadili rangi na mwonekano hali wa ngozi.

wanaume wapo hatarini kupata aina hii ya saratani mara tatu zaidi ya wanawake, kutokana na
sababu za kibailojia. Lakini sababu hatarishi za ugonjwa huu kwa ujumla wake ni kupigwa na
jua kwa muda mrefu zaidi.
Hivyo, inashauriwa kwa watu kupata vipimo vya ngozi vya mara kwa mara na hasa pale dalili
mbalimbali zinapojitokeza kwenye ngozi kama vile kubadilika kwa maumbile ya ngozi,
kubadilika kwa rangi ya ngozi, na kujitokeza kwa chunusi sugu mara kwa mara kwa kuwa hizi
ndizo dalili za saratani ya ngozi (melanoma).
Tiba ya magonjwa ya ngozi inaleta tija zaidi wakati ambapo vipimo vikifanywa kwa wakati na
kugundua tatizo.