Ndege za kivita za Israel zimeishambulia miji ya Beirut na Tehran leo huku kukiwa hakuna dalili ya kumalizika kwa vita vinavyoelekea kutimiza wiki nzima kesho Jumamosi.
Israel ilisema mapema asubuhi kuwa imefanya “mashambulizi makubwa” kwenye mji mkuu wa Iran na mashuhuda wameyaelezea mashambulizi hayo kuwa mazito na kwamba kwenye maeneo yalikolenga nyumba zilitikisika.
Israel imeyapiga pia maeneo kadhaa ya mji mkuu wa Lebanon kulikabili kundi la Hezbollah lenye mafungamano na Iran.
Tehran ilijibu mashambulizi hayo kwa kuvurumisha makombora kuelekea Israel, Kuwait, Qatar, Saudi Arabia, Bahrain na nchi zote zenye kambi za jeshi la Maekani.
Milipuko ilisikika kwenye mji wa Tel Aviv nchini Israel na kwenye mji mkuu wa Bahrain, Manama. Serikali ya Bahrain imesema majengo matatu ikiwemo moja la hoteli yamelengwa na makombora ya Iran.


