……………………………………………….

Na Hellen Mtereko,Mwanza

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Maendeleo ya Vijana, Dkt. Joel Nanauka amezindua programu ya kuwezesha mitaji kwa vijana watakaotekeleza miradi ya ufugaji samaki kwa njia ya vizimba.

Hafla hiyo imefanyika leo Jumamosi Machi 07, 2026 katika eneo la Feta lililoko Wilaya ya Nyamagana Jijini Mwanza.

Amesema miradi hiyo itatekelezwa katika mikoa ya Mwanza,Mara na Kagera pamoja na miradi ya ufugaji wa jongoo bahari,kilimo cha mwani na unenepeshaji wa kaa itakayotekelezwa ukanda wa Pwani hususani mikoa ya pwani na Mtwara.

“miradi hii ambayo ina dhana ya uchumi wa blue inanionesha wazi kuwa vijana wa kutanzania wanamchango mkubwa wa kusukuma mbele agenda ya Rais Dkt. Samia Suluhu ya kufanya mageuzi ya kisekta ili kukuza uchumi sambamba na Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050”, Amesema Dkt. Nanauka

Amesema Serikari itakuwa bega kwa bega na vijana huku akiwakumbusha kuwa waadilifu katika kusimamia mifumo na rasilimali wanazopewa.

Kwaupande wake Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Profesa Mohamed Sheikh, amesema katika mwaka wa fedha 2025/2026 Serikari kupitia wizara ya mifugo na uvuvi imetoa kiasi cha bilioni saba kwaajili ya kuwawezesha vijana wa BBT waliopata mafunzo kwa vitendo ya uvuvi na ukuzaji viumbe maji kupata mitaji ya kutekeleza miradi waliyoibuni wenywe.

Amesema mitaji hiyo itatolewa kwa njia ya mkopo wenye masharti nafuu ambapo fedha hizo zinatarajiwa kuwawezesha jumla ya vijana 308,kati ya vijana 486 waliohitimu.

“Kati ya vijana 308 watakaowezeshwa vijana 160 watatekeleza miradi ya ufugaji wa samaki kwenye vizimba na vijana 148 watatekeleza miradi ya ufugaji wa jongoo bahari,kilimo cha mwani pamoja na unenepeshaji wa kaa”, Amesema Profesa Sheikh

Aidha, amesema Wizara inapanga kutumia sehemu ya shilingi bilioni 23 ambazo imezipokea kwaajili ya kuwawezesha vijana zitumike kuwawezesha vijana wa BBT waliosalia.

Amesema vizimba vinauwezo wa kuchukua vifaranga 11,500 na kuzalisha wastani wa Tani 3.5 kwa kizimba katika kipindi cha miezi 7 kwa gharama ya shilingi 17,246,188.75.

“leo hii utazindua uwezeshaji wa mitaji kwa njia ya mkopo wenye masharti nafuu kwa vijana 55 ambao watapokea hundi ya mfano ya shilingi bilioni 7 (Dummy cheque kwa niaba ya vijana 308 ambao wamepangwa kuwezeshwa mitaji”,