Iran imetupilia mbali mpango wa Marekani wa kusitisha vita huko Mashariki ya Kati huku ikiendeleza mashambulizi zaidi dhidi ya Israel na nchi za Ghuba.

Tehran hata hivyo imesema inalipitia tena pendekezo hilo lakini Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Abbas Araghchi amesema Iran haina nia ya kufanya mazungumzo na wala haijashiriki katika mazungumzo yoyote ya kukomesha vita.

Kauli hiyo imetolewa baada ya Ikulu ya White House kusema kuwa rais wa Marekani Donald Trump yuko tayari kuisambaratisha Iran ikiwa itakataa kufikiwa kwa makubaliano. Araghchi ameendelea kuwa kwa sasa Iran imejijingea hadhi ya kutoweza kushambuliwa tena na kwamba maadui zao watahofia kuingia tena katika vita na watu wa Iran.