Na Cresencia Kapinga, JamhuriMedia, Ruvuma

UMOJA wa Mawakala wauzaji wa Pembejeo Mkoa wa Ruvuma (UWAPERU) wameishukuru Serikali kwa kutoa Ruzuku kwa wakulima ambapo katika msimu huu wa kilimo wakulima wamefaidika na ruzuku hiyo kwa kupata mbolea na kuongezea uzalishaji wa mazao.

Akifungua Mkutano wa umoja wa Mawakala wauza Pembejeo (UWAPERU) uliofanyika katika ukumbi wa mkutano wa Heritage cottage Manispaa ya Songea Leo April 9 /
2026,Rosemary Haule (Minjingu) alisema kuwa hawana budi kuishukuru serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania Dk. Samia Suluhu Hassan kwa kuwatengenezea mazingira mazuri ya kufanyia biashara na wakulima kwa kuuza mbegu ,viwatilifu na mbolea.

Aidha pamoja na shukrani hizo amesema kuwa wanakabiliwa na changamoto ya hupatikanaji wa baadhi ya pembejeo hususani Mbolea aina ya AS,CAN na UREA kwa wakulima ambao walichelewa kupanda msimu huu wa kilimo na kwa sasa wanahitaji huduma hiyo ya mbolea.

Upendo Mwakanosya mfanyabiashara na muuzaji wa pembejeo za kilimo wilayani Mbinga ameiomba serikali kuwasimamia makampuni ya usambazaji wa pembejeo TFRA,TOSCI na TPHPA kwani unakuta msimu wa kilimo unafika pembejeo hazipatikani kwa wakati kama msimu uliopita 2024/2025 mbolea za kupandia DAP zilichelewa jambo ambalo linasababisha kushuka kwa uzalishaji.

James Mlelwa (Sambala) alisema kuwa wakulima wengi wa Mkoa wa Ruvuma huwa wanapanda mazao kwa nyakati tofauti tofauti inapotokea changamoto ya ukosekanaji wa mbolea za kukuzia na kuzalisha inaleta shida hivyo ameiomba serikali kuwasaidia upatikanaji wa pembejeo hizo kwa haraka.

Mwenyekiti wa umoja wa Mawakala wauzaji pembejeo Mkoa wa Ruvuma (UWAPERU) Rosemary Haule