Dkt. Janet Lekashengo, Mwenyekiti wa Tume ya Madini ni moja ya viongozi mbalimbali wanaoendelea kutembelea Banda la Wizara ya Nishati katika maonesho ya Kimataifa ya Biashara (Sabasaba) yanayoendelea katika Viwanja vya Mwl.Nyerere jijini Dar es Salaam.
Katika banda la Wizara, ameelezwa kuhusu juhudi zinazoendelea kufanywa na Serikali katika usambazaji umeme katika maeneo ya migodi ikiwemo mpango wa kuwezesha uunganishaji umeme katika migodi midogo midogo iliyopo Chunya-Mbeya na Kwa Msisi-Handeni mkoani Tanga.







