Na Mary Margwe, JamhuriMedia, Mbulu
Mwenge wa Uhuru 2026 umezindua rasmi Jengo jipya la Utawala la Halmashauri ya Mji wa Mbulu lenye thamani ya ya zaidi ya bil. 3.4 hali inayolenga kuboresha mazingira ya kazi kwa watumishi wa umma na kuongeza ufanisi wa utoaji wa huduma kwa wananchi.
Aidha mradi wa jengo hilo limengwa katika Kata ya Sanu Baray, Mtaa wa Sanugwa, kiwanja na.115-122 lenye hati 35 MNY na kina ukubwa wa mita za mraba 12,645, Ujenzi wake ulianza utekelezwa Agosti 2023 na kukamilika Juni 30, 2026.
Kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya hiyo Michael Semindu taarifa hiyo ilisomwa mbele ya Kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru kitaifa 2026 Wazo Mwang’onda kuwa zaidi ya shi.bil. 2.52 zimetumika kwenye ujenzi, huku sh.mil. 300 zikitumika kwenye ununuzi wa samani.
” Lengo la mradi huu kuboresha mazingiraya kufanyia kazi Kwa watumishi na kuboresha utoaji wa huduma ya kiutawaka Kwa wananchi, ambapo jengo hililina ghorofa moja na Lima vyumba 72 pamoja kumbi mbili za mikutano” amesema Semindu.
Mradi huo umetekelezwa kwa utaratibu wa Force Account chini ya fundi Mjenzi SUMA JKT na tayari umeanza kutumika, ukitarajiwa kuimarisha uratibu wa shughuli za halmashauri na kurahisisha upatikanaji wa huduma mbalimbali za kiutawala kwa wananchi.
Akizungumza mara baada ya kuzindua jengo hilo, Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2026, Wazo Michael Mwang’onda, amesema uwekezaji unaofanywa na Serikali katika ujenzi wa miundombinu ya utawala unalenga kuongeza ufanisi wa utendaji wa watumishi na kuboresha huduma zinazotolewa kwa wananchi, huku akimpongeza Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri hiyo Rehema Bwasi kwa usimamizi mzuri na makini wa ujenzi huo.
“Miradi kama hii inaonyesha dhamira ya Serikali ya kuimarisha utawala na kuboresha huduma kwa wananchi. Ni wajibu wetu kuhakikisha miundombinu hii inalindwa na kutumika kwa manufaa ya vizazi vya sasa na vijavyo.”
Aidha, amesisitiza umuhimu wa kuendelea kudumisha amani, umoja na mshikamano ili kuweka mazingira bora ya maendeleo na kuhakikisha uwekezaji wa Serikali unaendelea kuwanufaisha wananchi.




