Na Mwandishi Wetu, JamhuriMedia, Dar es Salaam

Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Stephen Wasira, amejibu hoja ya Makamu wa Rais aliyejiuzulu, Balozi Dk. Emmanuel Nchimbi ya kuwataka Watanzania wapambanie Katiba Mpya.

Akizungumza Dar es Salaam leo Septemba 8, 2026 katika Mkutano wa Kitaifa wa Wadau Kutafakari Hali ya Kisiasa Nchini: Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025 na Mustakabali wa Taifa ulioandaliwa na Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD), amejibu kwa kuhoji: “Unataka watu wapambanie Katiba, wapambanie nini?”

Wasira ametoa kauli hiyo baada ya mtoa mada katika mkutano huo, Profesa Mshiriki, Ndaki ya Insia (College of Humanities), Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Elgidius Ichumbaki, kusema kwamba watu wanaozungumzia masuala ya wananchi wanashughulikiwa akitoa mfano wa Nchimbi.