*Nanauka asifu,apongeza Juhudi za Serikali kwa uwekezaji
*Atoa rai kwa vijana kushiriki kikamilifu kwenye uzalishaji viwandani.
Na Innocent Byarugaba -ORMV
Hivi karibuni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Maendeleo ya Vijana Mhe.Joel Arthur Nanauka amefanya ziara rasmi kujionea utekelezaji wa Mradi wa Ukanda maalum wa kiuchumi wa Benjamin William Mkapa (BWM-SEZ) ikiwa ni utekelezaji wa Dira ya Maendeleo ya Viwanda “the Tanzania Mini-tiger 2002” iliyofanikisha Maendeleo ya Uchumi wa Viwanda barani Asia
Mradi huu uliopo Mabibo External Jijini Dar es Salaam unatumia eneo lenye ukubwa wa hekta 25 ambao ni ekari 65 kwa lengo la kuchochea ukuaji wa sekta ya Viwanda,kukuza Mauzo ya bidhaa nje ya nchi na kutoa ajira kwa Vijana.
Akiwasilisha taarifa mbele ya Nanauka Michael,Kaimu Mkurugenzi Mkuu TISEZA amebainisha kuwa mradi umejengwa na Serikali kikamilifu kwa Dola za Marekani Milioni 29.862 sawa na Bilioni 36.4 kati ya Mwaka 2005-2010 ukihusisha miundombinu ya barabara, Maji, Umeme, Maji taka na Gesi na ulizinduliwa rasmi na Mhe.Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete Rais Mstaafu wa awamu ya nne.
Aidha, Michael akizungumzia hali ya uwekezaji ameeleza kuwa mpaka Agosti 31,2026 jumla ya Viwanda 14 vinavyojighulisha uzalishaji, uchakataji wa Mazao ya Kilimo, Uchakataji wa Chakula, Vifungashio,Wiwanda vya nguo na vingine vidogo vinafanya kazi ambapo mitaji yenye Dola za Marekani Milioni 114 kutoka ndani na nje ya Tanzania zimewekezwa huku Mauzo ya nje yakiwa zaidi ya Dola za Marekani Milioni 300.
Akizungumzia upande wa fursa na ajira kwa vijana, Michael amesema kuwa zaidi ya Vijana 8,000,000.00 za Moja kwa moja zimezalishwa ambao 85% ni Vijana wa Kitanzania ambapo kati ya Viwanda 14 Viwanda 2; Took Garments Company Limited imeajiri Vijana 6000 huku Afriport Apparel Limited ikiajiri Vijana takriban 300
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Maendeleo ya vijana Joel Nanauka ameridhishwa na Utekelezaji wa Mradi huo na kupongeza maono ya Viongozi wa Kitaifa kuanzisha mradi huo ambao leo ni kama tanuru la Uchumi kwa kwa Taifa huku likichangia fursa ajira kwa Vijana.
Nanauka amewapongeza wawekezaji wote kwa kuendeleza matamanio na shauku ya Serikali kuanzisha mradi huo hivyo kuwataka kuweka mazingira wezeshi na rafiki kwa Vijana wa Kitanzania kunufaika na uwekezaji huo.
Aidha,Mhe.Nanauka amempongeza Dkt.Samia Suluhu Hassan na Serikali yake ya awamu ya sita kwa kuendelea kutenga maeneo mengine maalum ya Kiuchumi yenye ekari 520 kwenye maeneo ya Bagamoyo ekari 50,Kwala ekari 20,Manyara Ekari 100,Nala ekari 100,Tanga ekari 100,Songea ekari 100 na Bunda ekari 20 kuwa yatakapo kamilika na Kuanza uzalishaji yataongeza wigo wa ajira kwa Vijana na kuongeza Pato la Taifa.
Nanauka ametoa rai kwa Vijana kuchangamkia fursa za ajira kwenye Viwanda na kufanya kazi weledi,Juhudi na maarifa, kwa Uzalendo ili kuweza kujikwamua kimaisha na sio kuwa vikwazo viwandani wanapoajiriwa.
Nanauka ametumia fursa hii Kumpongeza Waziri mwenye dhamana ya Viwanda na Uwekezaji Mhe.Prof.Kitila Alexander Mkumbo kwa usimamizi wa karibu wa Mradi huo ambao tija na matunda yake si tu yanalinufaisha Taifa kupitia Kodi bali mradi unawaneemesha vijana kupitia ajira.



