Balozi wa Tanzania nchini Oman, Mheshimiwa Maulida Hassan amewasilisha Hati za Utambulisho kwa Sultan, Mtukufu Haitham bin Tariq Al Said.
Tukio hilo lililofanyika katika Kasri la Al Hosni mjini Salalah limeakisi uhusiano wa karibu na wa kihistoria uliopo kati ya Tanzania na Oman.
Kwenye hafla hiyo, Mtukufu Haitham bin Tariq Al Said na Balozi Maulida wameombeana dua kutoka kwa Mungu ili kila mmoja aweze kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi.


