Na Mwandishi Wetu,JamhuriMedia, Dar es Salaam

Vijana chini ya umri wa miaka 17 (Serengeti Boys), itakayoiwakilisha nchi katika mashindano ya Kombe la Dunia, Nchini Quatari akisisitiza kuwa mafanikio ya timu hiyo ni matokeo ya uwekezaji na juhudi zinazofanyika katika kukuza sekta ya michezo nchini.

Akizungumza na Waandishi wa Habari leo Novemba 6,2026 Jijini Dar es salaam Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam RC Albert Chalimila amesema Timu hiyo imepangwa katika Kundi la Kwanza pamoja na timu za taifa za Brazil na Costa Rica, huku ikitarajiwa kushiriki mashindano hayo nchini Qatar, ambako itahitaji sapoti ya Watanzania ili kufanya vizuri na kuipeperusha vyema bendera ya taifa.

Amesema mafanikio ya Serengeti Boys kufuzu kwa mashindano hayo yanaendeleza historia nzuri ya soka la vijana nchini, baada ya timu hiyo kufanya vizuri katika fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kwa vijana chini ya miaka 17 zilizofanyika Morocco, ambako ilifika hatua ya fainali na kucheza dhidi ya Senegal.

Katika mchezo huo wa fainali, Tanzania ilipoteza kwa mikwaju ya penalti baada ya timu hizo kutoka sare ya bao 1-1 ndani ya muda wa kawaida wa mchezo.

Aidha, amesema Serikali itaendelea kuunga mkono timu hiyo, huku akieleza kuwa yeye pamoja na wakuu wa wilaya na viongozi wengine wataungana na Watanzania wachache watakaosafiri kwenda Qatar kuishangilia timu hiyo katika michezo yake.

Ameongeza kuwa Serikali itagharamia baadhi ya mashabiki watakaosafiri kwenda Qatar ili kuongeza hamasa na kuhakikisha vijana hao wanapata sapoti ya kutosha wanapokuwa uwanjani.

Rais Samia pia ametoa wito kwa viongozi na wadau mbalimbali, wakiwemo wanahabari, kushiriki katika kuhamasisha Watanzania kuiunga mkono timu hiyo, akisisitiza kuwa mafanikio ya michezo yanahitaji mshikamano wa jamii nzima.