Na Aziza Nangwa, Jamhuri Media
Serikali imeweka mpango wa kujenga barabara mbadala itakayounganisha Kigamboni, Kisarawe hadi Chalinze mkoani
Pwani,kwalengo la kupunguza msongamano wa magari ya mizigo yanayoingianakutoka katika Bandari ya Dar es Salaam.
Barabara hiyo inatarajiwa kuwa njia mbadala kwa malori yanayosafirisha mizigo, ili kupunguza matumizi ya barabara za Mandelana Morogoro ambazo zimekuwa zikibeba sehemu kubwa ya shughuli za usafirishaji jijini.
Akizungumzia mpango huo, kwenye mkutano wake na Waandishi wa habari uliofanyika katika hotel ya Johari Rotana Jiji Mkuu wa Mkoa wa Dar esSalaam, Albert Chalamila, ameema mkoa huo unatarajia kuwasilishamapendekezo ya mradi kwa kushirikiana na Mkoa wa Pwani pamoja naWizara ya Ujenzi.
Amesema ujenzi wa njia hiyo utasaidia kuboresha usafirishaji wa mizigo, kupunguza msongamano wa magari na kurahisisha shughuli zakiuchumi zinazotegemea bandari.
Katika hatua nyingine, Chalamila amesema Wilaya ya Temeke imetatoakata 10 zitakazotumika kwa shughuli za kimkakati zinazohusiana namnyororo wa thamani wa Bandari ya Dar es Salaam.
Amesema kuwa baadhi ya maeneo ya Kigamboni yaliyo karibu na matenki ya mafuta pia yanatarajiwa kujumuishwa katika mipango ya maendeleo inayohusiana na shughuli za bandari.
Alifafanua kuwa hatua hiyo kuwa sio uporaji wa ardhi, bali ni mpango wa kuweka matumizi bora ya ardhi kwa kuzingatia mahitaji ya maendeleona shughuli za kiuchumi katika maeneo yalio karibu na Bandari
‘’Mpango huo unatajwa kuwa sehemu ya juhudi za kuboresha miundombinu ya usafirishaji na kuongeza ufanisi wa shughuli za Bandari ya Dar es Salaam, ambayo ni miongoni mwa vituo muhimu vya biashara nchini.’’Amesema
Chalamila amesema mpango huo ukikamilika , barabara hiyo inatarajiwa kupunguza shinikizo la magari makubwa katika barabara kuu za jiji na kuboresha mtiririko wa usafiri kwa watumiaji wengine wa barabara za Morogoro road na Mandela road katika mkoa wa Dar es salaam.



