Na Mwandishi Wetu, JamuhuriMedia, Songea
Mdau wa maendeleo, Bi. Getrude Haule, amesema kuwa michezo ni nyenzo muhimu ya kuunganisha watu katika jamii bila kujali tofauti zao za kisiasa na kidini.
Getrude ameeleza hayo Jana wakati akifunga mashindano ya Mpira wa miguu yaliyoandaliwa na Jogoo cup yaliyofanyika kwenye viwanja vya michezo vya shule ya msingi Bombambi Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma.
Alisema kuwa michezo ina nafasi kubwa katika kujenga umoja, mshikamano, upendo na mahusiano mema miongoni mwa wananchi, kwani kupitia michezo watu kutoka makundi mbalimbali hukutana, kushirikiana na kujenga urafiki.
Amesema michezo haipaswi kuangaliwa kama shughuli ya burudani pekee, bali ni jukwaa muhimu linaloweza kutumika kuimarisha amani, kuondoa tofauti na kukuza ushirikiano katika jamii.
Aidha amewataka wananchi kujitokeza kwa wingi kumpokea makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Deogratius Ndejembi ambaye atawasili kesho mkoani Ruvuma kwaajiri ya ziara ya kikazi.







