Rais Dk Mwinyi aongoza wananchi katika mazishi ya marehemu Charles Hilary Zanzibar
JamhuriComments Off on Rais Dk Mwinyi aongoza wananchi katika mazishi ya marehemu Charles Hilary Zanzibar
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiweka shada la maua katika kaburi la aliyekuwa Mkurugenzi Mawasiliano Ikulu Zanzibar na Msemaji Mkuu wa Serikali Marehemu Charles Martin Hilary, maziko yaliyofanyika leo 14-5-2025 katika makaburi ya Mwanakwekwe Wilaya ya Magharibi “B” Unguja.(Picha na Ikulu).RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiweka mchanga katika kaburi la Marehemu Charles Martin Hilary, aliyekuwa Mkurugenzi Mawasiliano Ikulu Zanzibar na Msemaji Mkuu wa Serikali, yaliyofanyika leo 14-5-2025, katika makaburi ya Mwanakwerekwe Wilaya ya Magharibi “B” Unguja.(Picha na IkuluMJANE wa Marehemu Charles Martin Hilary aliyekuwa Mkurugenzi Mawasiliano Ikulu Zanzibar na Msemaji Mkuu wa Serikali.Bi.Sara Mwakajuki akiwa na Watoto wake akiwasili katika makaburi ya Mwanakwerekwe Wilaya ya Magharibi “B” Unguja yaliyofanyika leo 14-5-2025.(Picha na Ikulu)RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiwa na Mkewe Mama Mariam Mwinyi, wakitowa mkono wa pole kwa familia ya Marehemu Charles Martin Hilary, aliyekuwa Mkurugenzi Mawasiliano Ikulu Zanzibar na Msemaji Mkuu wa Serikali, baada ya kumalizika kwa hafla ya kuuaga mwili wa Marehemu, iliyofanyika katika viwanja vya Mapinduzi Square Michezani Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja leo 14-5-2025.(Picha na Ikulu)RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akizungumza wakati wa kuagwa kwa mwili wa Marehemu Charles Martin Hilary aliyekuwa Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu Zanzibar na Msemaji Mkuu wa Serikali, hafla hiyo iliyofanyika katika viwanja vya Mapinduzi Square Michezani Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja leo 14-5-2025.(Picha na Ikulu).BAADHI ya Wananchi na Viongozi wa Serikali wakiwa katika viwanja vya Mapinduzi Square Michezani Wilaya ya Mjini Unguja wakati wa kuuaga mwili wa Marehemu Charles Martin Hilary, aliyekuwa Mkurugenzi Mawasiliano Ikulu Zanzibar na Msemaji Mkuu wa Serikali, hafla hiyo iliyofanyika leo 14-5-2025.(Picha na Ikulu)RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akisaini kitabu cha maombolezi ya aliyekuwa Mkurugenzi Mawasiliano Ikulu Zanzibar na Msemaji wa Serikali Marehemu Charles Martin Hilary, wa hafla ya kuuaga mwili wa Marehemu iliyofanyika katika viwanja vya Mapinduzi Square Michezani Wilaya ya Mjini Unguja.(Picha na Ikulu)