Serikali imesema Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani mwaka 2025 utagharamiwa kwa fedha za ndani.
Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Fedha, Dk Mwigulu Nchemba, alipokuwa akiwasilisha makadirio ya mapato na matumizi ya Serikali kwa mwaka 2025/26 bungeni leo Juni 12, 2025.
“Mheshimiwa Spika, maeneo mengine mahsusi ya vipaumbele ni pamoja na ugharamiaji wa: Deni la Serikali; mishahara na stahiki za watumishi wa umma; pamoja na ujenzi na ukarabati wa viwanja vya michezo kwa ajili ya maandalizi ya michuano ya AFCON 2027.
“Aidha, nipende kuwafahamisha watanzania kuwa Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025 tutaugharamia kwa fedha zetu za ndani,” amesema Waziri Nchemba.
