Na Mary Margwe, JamhuriMedia, Dodoma
Viongozi wa Dini wilayani Kiteto Mkoani Manyara wamempongeza mbunge wa Jimbo hilo Wakili Msomi Edward Ole Lekaita kwa uwajibikaji wake katika kuwaletea Maendeleo wananchi wakem huku wakidai ni mbunge huyo ni Tumaini la wana-kiteto
Hayo yalibainishwa na Viongozi hao wa Dini walipokua Wakiongea kwa nyakati tofauti mara baada ya Viongozi hao kufanya ziara ya kutembelea Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kujionea shughuli mbalimbali zinazofanya na Bunge hilo, wamesema kuwa Wana Imani kubwa sana na mbunge mbunge huyo,miwani ni kiongozi mchapa kazi kweli kweli na hodari
Viongozi hao wamesema walichofurahishwa zaidi ni pale walipomuona Mbunge wa Jimbo hilo Edward Ole Lekaita alipouliza swali ” Ni lini Serikali itajenga Vituo vya Afya vya Kimkakati vya MATUI na DONGO katika Halmashauri ya wilaya ya kiteto”

Mchungaji wa kabisa la Free Pentecostal Church Of Tanzania ( FPCT ) Elia Aloyce Mkilanya amesema wamefurahishwa na mwaliko wa Mbunge kwenda kutembelea Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kuweza kuona namna mbunge huyo anavyopambania Maendeleo ya wanna Kiteto.
Mchungaji Mkilanya amesema wameshuhudua mbunge Lekaita akiuliza swali la kuikumbushia Serikali juu ya ujenzi wa Vituo vya Afya vya Kimkakati vya Matui na Dongo ambapo Naibu Waziri wa Tamisemi Dkt. Festo John Dugange amemjibu Mbunge Lekaita kuwa Serikali itajenga Vituo hivyo kwani Serikali inatambua uhitaji wa vituo hivyo kwa jamii hiyo na utaendelea kutenga kuhakikisha Vituo hivyo vinajengwa.
Mwenyekiti Mjumbe wa Baraza la Mashekh Wilaya Bakwata Sheikh Said Salim Mrumbi amesema Mbunge Lekaita amekua kiungo mkubwa wa Maendeleo katika jamii, maana toka alipoingia madarakani miradi mingi imeingia katika wilaya ya Kiteto, hivyo hilo ni ja,bo kubwa la kupongezwa.
” Sasa hivi kama tulivyomuona Mbunge wetu Bungeni amefuatilia ujenzi wa Vituo vya Afya vya Kimkakati vya Matui na Dongo, hakika hili ni hitaji letu kubwa sana kama Viongozi wa Dini Kiteto na ni Imani yetu kuwa Serikali yetu ya awamu ya sita chini ya mama yetu, Rais wetu Dkt. Samia Suluhu Hassan ataendelea kutukumbuka kwa miradi mingine kama hii na mingine pia, na hii itakamilika tu, kwani tunaye Mwakilishi wetu mchapa kazi kweli kweli na mfuatiliaji mzuri kuhakikisha Kiteto inasonga mbele kimaendeleo.

“Tunashukuru sana rais Dkt.Samia kwa kutuletea miradi inayoigusa jamii moja kwa moja, Mwenyezi Mungu aendelee kumbariki na kumpatia afya njema” amesema Sheikh Mrumbi.
Hata hivyo akiongea na Jamhuri Media Mbunge wa Jimbo hilo Wakili Msomi Edward Ole Lekaita amemshukuru Rais Dkt Samia kwa kuendelea kuwapatia Maendeleo Jimbo la Kiteto na hivyo kuahidi mitano tena kwa Rais Samia mwa uwajibikaji wake wa kuwaletea maendeleo Kiteto.
