KATIKA hali isiyo ya kawaida wabunge wa upinzani wamepiga kura ya ndiyo kwa bajeti Kuu ya Serikali hali iliyoibua shangwe kwa wabunge wa Chama cha Mapinzi kwa kuwapigia makofi yanayoashiria furaha yao kwa kitendo hicho.
Hali hiyo imejiri jana Bungeni jijini Dodoma wakati wa kumpitisha bajeti Kuu ya Serikali ambapo wabunge huitwa kwa jina moja moja kwa ajili ya kuitikia ndiyo au hapana ambapo hakukuwa na kura ya hapana hata moja.
Hatua hiyo imefanya bajeti hiyo ya 2025/2026 kupita kwa kishindo kwa asilimia 98.7.
Akitangaza matokeo ya upigaji kura ya bajeti hiyo, Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson, alisema jumla ya wabunge 378 walishiriki kupiga kura ambapo kura za ndiyo zilikuwa 373, hakuna kura ya hapana, na wabunge 5 hawakuamua.
Kupitishwa kwa bajeti hiyo ni hatua muhimu katika utekelezaji wa mipango ya maendeleo ya Taifa kwa mwaka ujao wa fedha, ikionyesha muafaka mkubwa miongoni mwa wabunge kuhusu vipaumbele vya serikali.
Aidha Vipaumbele vya Serikali katika mwaka unao wa fedha vilivyotajwa na Waziri wa Fedha Dkt.Mwigulu Nchemba aliposoma taarifa ya bajeti hiyo kwa mwaka ujao wa fedha alisema Serikali inatarajia kutekeleza vipaumbele
Amevitaja vipaumbele hivyo kuwa ni kugharimia uchaguzi mkuu wa mwaka huu ,maandalizi ya viwanja kwa ajili ya michango ya Afcon 2027.
Aidha alitaka vipaumbele vingine kuwa ni utekelezaji na uendelezaji wa miradi ya kimkakati,kuimarisha delta za uzalishaji ,rasilimaliwatu na kuboresha mazingira ya Biashara. Nchini.


Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), akijibu hoja mbalimbali za wabunge wa kuhitimisha Mapendekezo ya Serikali ya Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa Mwaka 2025/26, bungeni jijini Dodoma

Wabunge mbalimbali wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakiwapongeza Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) na Naibu wake, Mhe. Hamad Hassan Chande, baada ya wabunge hao kupitisha kwa kishindo makadirio ya mapato na matumizi ya Serikali ya Shilingi Trilioni 56.49 kwa mwaka 2025/26, ambapo zaidi ya wabunge 373 sawa na Asilimia 98.7 walipitisha kwa kura ya ndio.