Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akipokea Tuzo Maalum ya ‘Power of 100 Women Award kutoka kwa Uongozi wa Access Bank Group kutoka kwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya Access Tanzania Ndugu Protase Ishengoma Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 08 Julai, 2025. Tuzo hii ambayo hutolewa kila baada ya miaka mitano inalenga kutambua na kusherehekea wanawake wa Kiafrika wanaotoa michango ya mageuzi kwa mataifa na jamii zao, kuhamasisha na kuhimiza kizazi kijacho cha viongozi Wanawake katika bara zima la Afrika. Pia kupaza sauti za Wanawake katika kuleta maendeleo endelevu ya Kiuchumi na kijamii barani Afrika.