Chama cha ACT-Wazalendo kimemuandikia barua ya wazi Rais wa Uganda, Yoweri Museveni kikimtaka amuachie Mbunge Robert Kyagulanyi (Bobi Wine) na wabunge wengine wanaoshikiliwa na Polisi.

Kimemtaka Rais Museveni kuweka mbele haki za binadamu kuliko maslahi yake yanayohusiana na siasa na kuwa yeye kama kiongozi mkongwe anatakiwa kuonesha Demokrasia kubwa.

ACT-Wazalendo kimesema wabunge hao wanatakiwa kuachiwa ili wakapatiwe matibabu kutokana na majeraha waliyoyapata.

Chama hicho pia kimetoa angalizo kuwa Uganda bora haiwezi kupatikana kukiwa na ukiukwaji wa haki za binadamu na sheria nchini humo.

Please follow and like us:
Pin Share