Na Dotto Kwilasa, JamhuriMedia,Dodoma

SERIKALI inatarajia kupata sh.trilioni 1.2 kutoka kwa wadau mbalimbali kwa lengo la kuimarisha sekta ya mifugo, uvuvi na kilimo.

Fedha hizo zimepatikaa kupitia Mkutano Mkuu wa Mifumo ya Chakula ya Afrika (AGRF) uliofanyika Septemba, mwaka huu, uliokutanisha viongozi wa serikali, wanasayansi, wawekezaji, watunga sera, wakulima na vijana kutoka mataifa zaidi ya 70

Hayo ymebainishwa jijini hapa leo Oktoba 2,2023 na Waziri wa Uvuvi na Mifugo Abdallah Ulega wakati akizungumza na wandishi wa habari kuhusu mafanikio ya iliyopata Tanzania kupitia mkutano wa AGRF.

“Katika mkutao wa AGFR uliofanyika Septemba mwaka huu Tanzania ilipata fursa ya kuonesha program bunifu ya BBT na kufanikiwa kupata sh.Trilioni 1.2 kama ahadi kwa ajili ya kufadhili programu katika sekta za kilimo, mifugo na uvuvi,”amesema.

Katika hatua nyingine Ulega amesema Serikali ya awamu ya sita imeweka mazingira rafiki kwa wawekezaji na kushirikiana nao katika kila hatua kwani Tanzania ina rasilimali, ardhi, na mazingira yanayofaa kwa shughuli za mifugo na uvuvi.

Amesema Septemba 5-8, mwaka huu anga la Tanzania lilijaa mazungumzo kuhusu mustakabali wa mfumo wa chakula barani Afrika kwenye mkutano wa AGFR.

Ulega amefafanua kuwa mkutano huo uliongozwa kwa uangalifu na Rais Dk. Samia ambapo kulikuwa majadiliano ambayo yalijikita katika mifumo tofauti ya chakula pamoja na minyororo yake ya thamani, mchango na uwezeshaji wa vijana na wanawake.

“Natoa shukrani zangu za dhati kwa Rais Dk. Samia kwa uongozi wake wenye mtazamo wa mbali. Dhamira na uadilifu wake vilivyoleta hadhi kubwa kwa jukwaa hili na kufanya liwe kubwa na, bila shaka, lenye mafanikio makubwa zaidi kuhusu mifumo ya chakula katika ardhi ya Afrika,

Aliongeza kuwa :”Chini ya ulinzi wake, Tanzania ilikuwa kitovu cha majadiliano ya mageuzi ambayo yataunda mustakabali wa bara letu,”

Katika hatua nyingine alieleza kuwa mkutano huo ulikutanisha wadau 5,400 kutoka nchi 90, ulionyesha ushirikiano wa kimataifa ulioimarika wa Tanzania.

Amefafanua kuwa sSekta ya mifugo inachangia takribani asilimia 7.4 ya Pato la Taifa la Tanzania ambapo watu milioni 10 wanajihusisha na ufugaji na uvuvi, ikiwa ni pamoja na wafugaji, wakulima wadogo, na wafugaji wa kibiashara.

“Sekta hii inachangia zaidi ya asilimia 1.5 ya pato la Taifa, na ina jukumu kubwa katika usalama wa chakula na lishe ya taifa. Tanzania, kama bara zima la Afrika, inakabiliwa na changamoto za mabadiliko ya hali ya hewa, rasilimali finyu, mazingira dhaifu, na ushindani wa masoko.

By Jamhuri