Kampuni ya Bharti Airtel inayomiliki Airtel Tanzania imeeleza kusikitishwa kwake na taarifa ya Waziri wa Mpango kuhusu umiliki wa kampuni hiyo kutokuwa halali. Bharti imesema, uwekezaji wake ulifuata na kuzingatia sheria na taratibu zote za nchi.

Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango

Ikumbukwe siku chache zilizopita waziri Mpango alipeleka taarifa ya kamati aliyoiunda kuchunguza umiliki wa kampuni ya simu Airtel kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli aliyeagiza kufanyika kwa uchunguzi huo tarehe 20 Desemba, 2017.
Baada ya kuwasilisha taarifa hiyo, Dkt. Mpango alisema Serikali imejiridhisha kuwa ubinafsishaji wa Shirika la Simu Tanzania (TTCL) kwenda Celtel, baadaye kuhamishiwa Zain na sasa Airtel ulifanyika kwa ukiukwaji mkubwa wa sheria, kanuni na taratibu.
Kufuatia ukiukwaji huo Dkt. Mpango amesema Serikali inayomiliki asilimia 40 ya hisa za kampuni ya Airtel imeamua kufanya mazungumzo na kampuni ya Airtel inayomiliki asilimia 60 ya hisa ili nchi iweze kupata haki yake.

By Jamhuri