Ajali yaua saba na kujeruhi kumi Bagamoyo

Watu saba wamefariki dunia na wengine kumi kujeruhiwa katika ajali ya gari ya abiria aina ya Coster iliyogongana uso kwa uso na gari ya mizigo aina ya Canter maeneo ya kiwangwa Bagamoyo leo asubuhi Januari 9, 2023.

Mmoja wa majeruhi akiongea na Jamhuri Digital amehusisha chanzo cha ajali hiyo na uzembe, kuwa dereva wa gari la abiria Coaster alikuwa akiendesha kwa mwendo mkali na kujaribu ku – “Overtake” gari lingine ndipo akagongana na gari la mizigo na kusababisha vifo vya watu watatu papo kwa hapo.

Dereva wa gari la mizigo na abiria wengine watatu wamefariki mara baada ya kufikishwa katika hospitali ya bagamoyo .

Majeruhi wanaendelea na matibabu hospitalini hapo.

8