Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo ametoa wito kwa Watanzania kutunza mazingira na kudumisha amani.

Ametoa wito huo leo Januari 08, 2023 wakati akizindua vyumba vya madarasa 12 na ujenzi wa uzio wa skuli ya sekondari ya Piki wilayani Wete – Pemba.

Amesema ni muhimu kulinda mazingira ili kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi yanayoikabili nchi yetu.

Akizungunza wakati wa hafla ya uzinduzi, Dkt. Jafo amewataka wanafunzi na jamii kwa ujumla kutunza miundombinu hiyo ambayo imejengwa kwa ubora na ustadi mkubwa.

Ujenzi huo umejengwa kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) ukiwa na gharama ya Sh.milioni 328.

Uzinduzi huo umefanyika katika wiki hii ya Maadhimisho ya miaka 59 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.