Halima Mdee Anena Kuhusu Uuzwaji wa Nyumba za Serikali

Mbunge wa CHADEMA Jimbo la Kawe Halima Mdee leo kupitia kwenye ukurasa wake wa Kijamii wa Twitter amesema uuzwaji wa nyumba za serikali ni miongoni mwa mambo ya Kifisadi yaliyowahi kutokea na yanayoendelea kuligharimu Taifa.
Halima Mdee aliongeza kusema kuwa watumishi wenye Stahiki ya kupewa Nyumba wanapangishiwa au kuishi hotel kwa gharama kubwa!
Hivyo amewataka wahusika wote waliofanya na wanaoendelea kufanya hivyo kuwekwa wazi ili hali hiyo isijitokeze na kushughurikiwa kwa mujibu wa sheria za nchi.