SIKU moja baada ya NEC kuanika majina ya wagombe huku jina lake likitajwa kuwa miongoni mwao, Djumbe Joseph aliyepitishwa na (NEC) kugombea ubunge Jimbo la Singida Kaskazini kwa tiketi ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), ameandika barua ya kujitoa katika uchaguzi mdogo ambao unatarajiwa kufanyika Januari 13, 2018 kwa kile alichosema anafuata msimamo wa chama chake.

Akizungumza na waandishi wa habari Djumbe amesema kuwa ameamua kuungana na viongozi wakuu wa chama chake kutoshiriki katika uchaguzi huo mdogo ambao unategemewa kufanyika mapema Januari 2018.

Chadema jana kilitangaza kuwa hakiweka muakilishi yoyote kugombea jimbo hilo la Singida Kaskazini kwa kile walichosema awali kuwa hawawezi kushiriki uchaguzi huo wa marudio bila tathimini kufanyika juu ya uchaguzi wa udiwani uliofanyika hivi karibuni ambao walidai ulitawaliwa na uvunjwaji wa haki na sheria.