RAIS Dkt. John Magufuli ametoa agizo kwa Mamlaka ya Takwimu ya Taifa (NBS) kuwachukuliwa hatua haraka mashirika, taasisi na watu wanaotoa takwimu potofu kuhusu ukuaji wa uchumi wa nchi na mambo mengine ya serikali ikiwemo kuwakamata na kuwafikisha mahakamani. 

Wanaosema vyuma vimebana vitaendelea kubama kweli kweli lakini wananchi wa Lindi na Mtwara wameamua kufanya kazi, kwao vyuma havitakaza kutokana na kupanda kwa bei ya Korosho. Nasikia wanawanywesha Mbuzi bia.

Nyumba zimeanza kushuka bei Dar, walikuwa wanalipisha kwa Dola, nyumba hizo lwamezikimbia. Tusitake kutangaza kuwa vyuma vimekaza kwa nia mbaya, watu hao muwapuuze.

Watu wanaolalamika eti vyuma vimebanwa vitabanwa kweli kweli. Tutabana vichwa, miguu, matumbo, tutabana kila kitu.

Ninawaomba Watanzania mpuuze uzushi unaoendelea kwenye mitandao ya kijamii kwamba uchumi umeshuka. Tumieni takwimu zilizokusanywa na ofisi ya takwimu ya taifa. Achaneni na wanaosema vyuma vimekaza, tumelegeza kwa wananchi wa kawaida.

Ili takwimu ziwe muhimu basi ziwe sahihi. Naendelea kusisitiza Taasisi ya Takwimu kuendelea kutoa takwimu sahihi. Natoa onyo kwa watu wanaotoa takwimu za uongo, naagiza mamlaka husika kuchukua hatua mara moja kwa watu wa namna hiyo.

Ninaomba kutoa onyo hasa kwa wale ambao wanakuja na takwimu zao za mifukoni. Mamlaka husika mtumie sheria zilizopo kuwabana wale ambao wanataka kuwapotosha Watanzania kwa takwimu zao za uongo. Ukukosea kutoa takwimu…umeichafua nchi”

Kifungu cha sheria kinasema atakayepotosha takwimu adhabu ni kifungo cha kuanzia miezi sita hadi miaka mitatu. Au faini ya Millioni moja hadi millioni kumi au vyote kwa pamoja. Tena mimi ningekuwa Jaji hii ya mwisho ndio ningetekeleza.

Niwaombe vyombo vya habari na wataalam wa mitandao, muwaone wataaalm wanaohusika na takwimu, tusitafute takwimu za kupika.

Natoa agizo, akitokea mtu anatoa taarifa za uongo na ikathibitika kweli amepotosha, chukueni hatua haraka. Awekwe mahabusu ili aendelee kujifunza namna ya kutoa takwimu sahihi,” alisema Magufuli.

By Jamhuri