Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA), leo Novemba 23, 2023 limetangaza matokeo ya mtihani wa darasa la saba uliofanyika Septemba 13- 14 mwaka huu.

Katika matokeo hayo jumla ya watahiniwa 1, 092, 960 sawa na asilimia 80.58 ya watahiniwa 1, 356, 296 wenye matokeo ya Mitihani wa Kumaliza Elimu ya Msingi 2023 wamefaulu ambapo wamepata madaraja ya A, B na C.

Akitangaza matokeo hayo Katibu Mtendaji wa NECTA Dk Said Mohamed amesema amefuta matokeo ya wanafunzi 31 kwa udanganyifu.

Pia amesema wanafunzi 360 ambaao walipata matatizo ya kiafya na kushindwa kufanya mitihani yote au idadi kubwa ya masomo watarudia tena mwaka 2024.

MATOKEO HAYA HAPA

By Jamhuri