Arsenal wameilazimisha sare ya 0-0 Chelsea katika uwanja wa Stamford Bridge Alexis Sanchez akianzia benchi na Wilshere akipata majeraha

Meneja wa Arsenal, Arsene Wenger amesisitiza kuwa uamuzi wake kumwanzisha Alexis Sanchez benchi kwenye mechi za Kombe la EFL dhidi ya Chelsea haukuwa na maana yoyote kuhusu uhamisho.

Mchezaji huyo wa kimataifa wa Chile, ambaye mkataba wake unakwisha Arsenal majira ya joto, amekuwa akihusishwa na tetesi za kutaka kuhama kwa miezi 12 sasa.

Sanchez alikuwa miongoni mwa wachezaji wa akiba Arsenal ilipoilazimisha sare Chelsea kwenye mechi ya kwanza nusu fainali katika uwanja wa Stamford Bridge lakini aliingia kuchukua nafasi ya Alexandre Lacazette dakika ya 66.

 Akiongea na BBC Sport baada ya mechi hiyo ya Jumatano usiku, ambayo ilimalizika bila goli, Wenger alidai kuwa kutolewa kwa Sanchez kikosi cha kwanza ni mbinu za kifundi.

“Nilifikiria kumwingiza baada ya saa moja,” Mfaransa huyo alisema. “Nilitambua kwamba tulihitaji kukaba zaidi na angeweza kubadili mchezo dakika 30 za mwisho. Lakini hakuna maana yoyote kuhusu uhamisho.”

Sanchez amekuwa akihusishwa sana na tetesi za kujiunga na vinara wa Premier League Manchester City.

Please follow and like us:
Pin Share