Mkurugenzi wa Mashtaka Nchini (DPP), Biswalo Mganga amelifunga rasmi jalada la kesi ya aliyekuwa mwanafunzi wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), Akwilina Akwilin (22).

Alisema kuwa, alipokea jalada la kesi ya askari sita waliokuwa wakishikiliwa na Jeshi la Polisi kutokana ana tukio linalodaiwa mwanafunzi Akwilina alipigwa risasi na kufa akiwa kwenye daladala wakati walipokuwa akiwatawanya wafuasi wa CHADEMA waliokuwa wamekusanyika eneo la Mkwajuni , Kinondoni, jijibi Dar es Salaam.

Alisema hakuna askari ambaye atashtakiwa kwa tukio lolote litakalotokea wakati akitekeleza kazi yake ya kuzuia ghasia au kuzuia maandamano.

“Labda niseme wazi, jalada la kesi hiyo nililipokea na nilishafanya maamuzi. huwezi kuniambia nani aliua pale kwa sababu kulikuwa na wau wengi na hawakukaguliwa, tutajua ni nani alikuwa na silaha na nani hakuwa nayo?” alihoji DPP.

Mganga alisema hata hivyo polisi hawawezi kuacha amani ivunjwe na hawawezi kuwajibika kwa lolote litakalotokea wakati wa kutkeleza kazi zao, ikiwemo kuzuia vurugu.

Kuhusu askari sita waliokuwa wanashikiliwa kwa tuhuma za mauaji hayo, Mganga alisema kama jalada limeshafungwa na askari wameachiwa huru hawana hatia.

Please follow and like us:
Pin Share