Na Mwandishi Wetu , Jeshi la Polisi- Dar es Salaam
Askari wa Jeshi la Polisi waliotimiza miaka tisa (09) kazini depo ya mwaka 2013/2014 (H3) wameguwa na Kampeni ya Namthamini inayoendeshwa na kituo cha Televisheni na Redio cha East Afrika ambacho kinalenga kuwasaidia watoto wa kike walioko shuleni kupata taulo za kike.
Akizungumza mara baada ya kukabidhi taulo hizo mkufunzi wa chuo cha Taaluma ya Polisi Daer es Salaam (DPA) ambae aliambatana na askari hao Mkaguzi wa Jeshi la Polisi INSP. Lule Mlay amebainisha kuwa askari hao wameungana ikiwa ni sehemu ya kumshukuru Mungu kwa kufikia miaka tisa ya utumishi ndani ya jeshi hilo huku akisema wametoa taulo za kike ili kusaidia kundi la mabinti walioko mashuleni.
Kwa upande wake mwanafunzi wa kozi ya mkaguzi msaidizi wa Polisi Digna Miho, amesema wameamua kumshukuru Mungu kwa kulikumbuka kundi la mabinti waliopo shuleni huku akibainisha kuwa anafahamu changamoto za mabinti wanapokuwa katika mizunguko ya mwezi (hedhi).
Nae mwanafunzi wa kozi ya Mkaguzi Msaidizi wa Polisi Abel Paul amesema mabinti wanahitaji kusoma bila kukutana na vikwazo kwa kutambua hilo waliona waungane na Kampeni ya Namthamini kuwasaidia mabinti kwa kutoa taulo za kike.