Na Byarugaba Innocent, JamhuriMedia, Kibaha

Leo Jumamosi Septemba 16,2023 Mkuu wa Wilaya ya Kibaha Nickson John, amewaongoza mamia ya wananchi kuadhimisha Siku ya Usafishaji kwa kufanya usafi kwenye Soko la Loliondo kuanzia Saa 12 hadi saa 4 Asubuhi.

Pamoja na mambo mengine Simon ametoa rai kwa wananchi kuwa na utamaduni wa kufanya usafi kwenye makazi yao pamoja na sehemu za biashara ili kuimarisha ustawi wa afya zao kwani uchafu na chakula hayaendani.

Asumpta Maziku ambaye ni mfanyabiashara wa nguo kwenye Soko hilo amewakumbusha wenzake kujiwekea utaratibu rafiki wa kusafisha Mazingira kwani uwepo wa Mazingira machafu huwakimbiza hata wateja kwa kuhofia kuhatarisha afya zao

Mwenyekiti wa mama lishe Sauda Hassan amesema kuanzia sasa mama lishe wataanza kutekeleza zoezi la usafi kwa vitendo ambapo kila mama lishe atapaswa kuwa na vyombo maalum vya kuhifadhia taka huku Mkuu wa Wilaya akiwataka wote ambao hawataweza kwenye falsafa ya usafi kuwapisha wengine wanaoweza kuendelea kujitafutia riziki eneo Hilo ambalo limeajiri akina Mama wengi.

“Wasiofanya usafi usafi wataondolewa,ni jambo la kusikitisha Sana,tena la aibu kwa sehemu ya Chakula kuwa chafu.Mama lishe asiyeweza kwenda na kasi ya usafi, atupishe”alisema Simon.

Aidha,Simon ametoa wito kwa Mkurugenzi kuhakikisha Sheria ndogondogo zinaimarishwa hasa faini za ukusanyaji taka,uzoaji,ulipiaji na upelekaji dampo ili kuendana na wakati wa Sasa na kuimarisha kwa misingi ya usafishaji Mazingira.

Diwani wa Kata ya Tangini Mfalme Kabuga ametoa rai kwa wafanyabiashara na wananchi wa Kata ya Tangini kufuata Sheria na kwamba yeyote atakaidi hatua za Kisheria zitachukuliwa.

Kila Septemba 16 ya kila mwaka Dunia hushiriki kwenye zoezi la usafishaji ikiwa ni ishara ya kukabiliana na Uchafuzi wa uharibifu wa mazingira.

By Jamhuri