Askofu mkuu wa kanisa la Full Gospel Bible fellowship (FGBF) Zakary Kakobe amesema haofii kuchunguzwa na serikali kuhusiana na ukwasi anaoumiliki na kuongeza kuwa fedha alizonazo ni Zaidi ya fedha zinazomilikiwa na serikali nyingi Duniani.

Akizungumza wakati wa ibada ya Jumapili kanisani hapo Askofu Kakobe amesema kuwa, hana wasiwasi wa kuchunguzwa utajiri wake na kuongeza kuwa kwa sasa anamiliki pesa nyingi Zaidi ya serikali ya China na Marekani.

Wiki iliyopita askofu Kakobe akihubiri wakati wa mkesha wa sikukuu ya Christmas alidai kuwa yeye ni tajiri zaidi ya serikali ya Tanzania na haogopi kusema ukweli.

Kauli hiyo ya askofu Kakobe ilipata upinzani mkali kutoka kwa wafuasi na viongozi wa CCM lakini ikapata uungwaji mkono kutoka kwa wafuasi wa upinzani.

Katika mahubiri yah ii leo Askofu Kakobe amewaambia waumini wake kuwa utajiri anaomiliki kwa sasa ni Zaidi ya serikali nyingi Duniani.

By Jamhuri