Azam FC imewaua kiume Simba 2-1 kwenye mchezo wa hatua ya nusu fainali Kombe la Azam Sports Federation mchezo uliochezwa Uwanja wa Nangwada Sijaona.

Ni Lusajo Mwaikenda dakika ya 22 alianza kupachika bao kwa Azam FC kisha usawa ukawekwa na Sadio Kanoute wa Simba dakika ya 27.

Muuaji ni Prince Dube dakika ya 73 akiwa ndani ya 18 alimtungua kipa namba tatu wa Simba, Ally Salim likiwa ni bao la ushindi.

Ngoma imegota mwisho kwa Simba 1 wakiwa hawana matumaini ya kutwaa taji lolote kwa msimu wa 2022/23 huku wachezaji wake wengi wakionekana kutokuwa kwenye mwendo mzuri.

Azam FC inatinga hatua ya fainali inasmubiri mshindi kati ya Singida Big Stars v Yanga mchezo utakaochezwa Uwanja wa Liti.