Na Isri Mohamed, JamhuriMedia, Dar es Salaam

BAADA ya gumzo la muda mrefu kila mmoja kiazungumza lake, hatimaye Klabu ya Yanga leo Julai 10, 2024 imethibitisha rasmi kuwa mchezaji wao Aziz Ki bado ataendelea kusalia klabuni kwako.

Baada tu ya kutamatika kwa kandarasi yake Yanga, kiungo huyo mshambuliaji raia wa Burkinafaso amekuwa akihusishwa na vilabu akdhaa ikiwemo Mamelod Sundowns ya Afrika Kusini ambao wanadaiwa kumuwekea kitita cha kutosha.

Mapema leo Yanga walitangaza kuwa mchezaji huo angezungumza na mashabiki wao majira ya saa 8 mchana, ambapo amethibitisha kwa kinywa chake mwenyewe kuwa bado ataendelea kuvaa jezi ya kijani na njano kwa msimu mwingine ujao.

Aziz Ki ndiye kinara wa mabao kwenye ligi kuu msimu uliopita akiwa na mabao Zaidi ya 20, huku akihusika kwa kiasi kikubwa kuifanya Yanga ichukue ubingwa, sambamba na kufanya vizuri kwenye michuano ya kimataifa.