Na Magrethy Katengu, JamhuriMedia, Dar es Salaam

Waziri wa Fedha na Mipango, Mwigulu Nchemba amesema Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Dkt. Samia Suluhu Hassan, imesikia kilio watumishi wa umma na wastaafu kuhusu kikokotoo na imekifanyia kazi kwa maslahi mapana ya wanaotarajiwa kustaafu.

Yamebaishwa hayo bungeni wakati Waziri huyo akiwasilisha bajeti ya mwaka 2024/ 2025 ambapo Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ameelekeza kuongezwa malipo ya mkupuo kutoka asilimia 33 iliopo sasa hadi
asilimia 40.

Sambamba na hayo Serikali imeendelea kuhakikisha kuwa malimbikizo ya kimshahara na yasiyo ya kimshahara ya watumishi wa umma yanalipwa kwa wakati ambapo katika kpindi cha miaka mitatu ya Serikali ya Awamu ya Sita, jumla ya shilingi bilioni 98.63 zimelipwa

Aidha, katika kipindi watumishi wa umma Serikali imelipa jumla ya shilingi bilioni 160.04 kwa ajili ya kugharamia upandishwaji wa vyeo kwa watumishi wa umma wapatao 126,814 katika kada mbalimbali

” Kuhusu kilio kikubwa kutoka kwa wastaafu kuhusu kikokotoo. Kama asemavyo Naibu Waziri wa Fedha Mheshimiwa Chande kuwa mara zote mtoto akilia mama hujua kwa sauti kuwa hapo mtoto analilia nini.

“Hivyo mabadiliko ya kikokotoo yalishusha kundi la wafanyakazi waliokuwa wakipokea mkupuo wa asilimia 50 mpaka asilimia 33 , na kundi waliokuwa wakipokea asilimia 25 walipandishwa mpaka asilimia 33” amesema Waziri.

Hivyo ndio kundi kubwa la watumishi wanaofanya mazi nzuri sana kwa taifa letu wakiwemo Walimu, kada ya afya, Polisi, Magereza, Uhamiaji, Zimamoto na makundi
mengine yalioko Serikali Kuu na Serikali za Mitaa Mheshimiwa Rais ameelekeza kuongezewa zaidi kundi lililokuwa likipokea asilimia 25 hapo awali na kupandishwa
kwenda asilimia 33 sasa itakuwa asilimia 35 kuanzia mwaka wa fedha huu na Watumishi takriban 17 walioathirika na mabadiliko
haya watazingatiwa katika mabadiliko haya. Serikali